Huduma ya walimu wa watoto
Astashahada ya walimu wa watoto na shule ya awali imelenga kuwaandaa watumishi kwa ajili ya kufundisha watoto makanisani na pia katika shule za awali.
Chuo cha Biblia Mbeya ambacho kwa sasa kinaitwa Southern Bible College ndicho chuo cha kwanza kuanzishwa katika kanisa la Tanzania Assemblies of God. Kilianzishwa na Mmishenari Wesley Hurst mwaka 1954.
Astashahada ya walimu wa watoto na shule ya awali imelenga kuwaandaa watumishi kwa ajili ya kufundisha watoto makanisani na pia katika shule za awali.
Shahada hii hutolewa muda wa jioni na kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Global University.
Stashahada ya Huduma na Biblia hutolewa kwa miaka 2 kwa waliopita chuo cha kupanda makanisa na miaka 3 kwa wasiopita chuo cha kupanda makanisa
BA The, MDiv.
Mkuu wa Chuo
Adv. Dip. The, BA Theo. MA Psychology
Mkuu wa Taaluma
Dip. Theo, BA Theo.
Msajili wa Chuo
Dip. Theo, BA Theo.
Meneja Shughuli
Dip. Theo. BA Theol.
Mshauri wa Wanafunzi
Adv. Dip. Children ministry Dip. Theo
Mratibu Huduma ya Mtoto
“Kila mtumishi na mwanafunzi katika Chuo cha TAG Southern Bible College atadhihirisha uaminifu wake kwa Mungu kwa kuishi maisha ya utakatifu, uadilifu pamoja na nidhamu ya kiroho katika maeneo yote ya maisha na utumishi wake.” — Utakatifu & Uadilifu
“Kila Mtumishi na Mwanafunzi katika chuo aamini Maandiko Matakatifu yamevuviwa na Mungu na ni ufunuo kwa mwanadamu na ni Kiongozi cha Imani kisichoshindwa wala kubadilika.” —Uaminifu kwa Biblia
“Kila mtumishi na mwanafunzi atakuwa wakili mwaminifu kwa kufuata na kutii kanuni na sharia zinazomhusu. ” — Uwajibikaji
“Kila mtumishi na mwanafunzi atakuwa na mahusiano yanayoonesha upendo na nia moja inayowezesha kufanya kazi kama timu kwa manufaa ya wote na kwa utukufu wa Mungu. ” — Kufanya kazi kama timu
“Kila mtumishi na mwanafunzi atadumisha uhusiano wa karibu na Mungu kwa kumsifu na kwa kumwabudu na kuwa na mahusiano naye kwa njia ya kumsikiliza kupitia Neno na Maombi.” — Ibada
“Kila mtumishi na mwanafunzi atafanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kupata matokeo bora ya kazi.” — Ufanisi